Je, unatamani kusafiri kwenda Bali, ili uweze kupiga picha nzuri kwa ajili ya Instagram? Au kutaka kununua gari au nyumba ili kuweza kulingana na maisha mazuri? Pamoja na watumiaji zaidi ya bilioni moja, kuonyeshana mambo muhimu kwenye mitandao yao ya kijamii kama Facebook, Youtube na Instagram si rahisi kutokudondokea kwenye mtego wa kulinganisha ambao husababisha watu wengi kushindana ‘likes’. Hakuna shaka juu ya hilo: mitandao ya kijamii inaathiri maamuzi makubwa ya kimaisha, na hata mifuko yako.
Kwa mujibu wa utafiti wa ‘Modern Wealth 2019’ uliofanywa na Charles Schwab, watu wanatumia zaidi ya uwezo wao ili kufurahia maono wanayoona kwenye mitandao ya kijamii.
Athari:
Uchunguzi wa kila mwaka unachunguza jinsi wamarekani 1,000 wenye umri wa miaka 21-75 wanafikiria kuhusu kujiwekea fedha, kutumia, kuwekeza na utajiri. Zaidi ya nusu ya wamarekani wanavutiwa na jinsi marafiki zao hutumia fedha ikilinganishwa na jinsi wanavyohifadhi, wakati asilimia 72 ya watu wa rika wanajiuliza jinsi marafiki zao wanaweza kupata uzoefu wa vitu vya gharama wanavyovituma katika mitandao ya kijamii.
Je, vyombo vya habari vya kijamii ni tatizo kwa wale ambao wanataka kujenga thamani yao halisi? Inaweza kuwa. Waliohojiwa wakati wa utafiti wanataja vyombo vya habari vya kijamii kama ushawishi mkubwa “mbaya” kwenye malengo yao ya usimamizi wa fedha.
Katika dunia ya kisasa, watu wengi wanapima mafanikio yao ya kifedha kulingana na uzoefu wanaoweza kumudu na vitu ambavyo wanaweza kutumia. Wamarekani wanaamini inachukua thamani ya dola milioni 2.3 kwa thamani ya mtu binafsi kuchukuliwa kuwa “tajiri,” kulingana na utafiti huo.
“Ufafanuzi wa zamani wa utajiri unazingatia kiasi cha dola ambacho si rahisi kwa watu wengi kukipata,” Alisema Abel Oonnoonny, Mshauri wa kifedha katika tawi la Charles Schwab huko New York City. “Mbinu ya kisasa ya utajiri imejikita katika shauku na uzoefu. Hayo ni malengo muhimu zaidi ya kifedha kwa wateja kuliko idadi”
Washiriki katika uchunguzi huo wameulizwa nini watafanya kuhusu kushuka kwa dola milioni 1 na matumizi makuu matatu ya fedha ni pamoja na umiliki wa nyumba, ununuzi wa gari, na malengo ya kusafiri.
Oonnoonny anaelezea presha ya “kwenda sawa na wakina Joneses ambayo imeongezeka kutokana na mitandao ya kijamii, lakini huna haja ya kuweka fedha zako zote za matumizi ili kufikia malengo ya kifedha “Kutumia sio adui, lakini ni muhimu kusawazisha fedha zinazotunzwa na kutumika ili kuweza kufurahia maisha na kufikia malengo ya muda mrefu ya kifedha kwa usalama.
Ikiwa unataka kuzuia kelele ya mambo ya kisasa na kuepuka tabia mbaya ambazo huja na mitandao ya kijamii, unapaswa kuunda mpango wa kifedha. Uchunguzi umeonyesha kuwa wale ambao wanaandika malengo yao chini wana nafasi nzuri ya kuyafanya malengo hayo na kuyafikia, lakini utafiti unaonyesha kuwa 28% ya Wamarekani wana mpango wa kifedha kwa kuandika. Kwahiyo, mpango wako mwingine wa kujikinga ni nini? fanya kazi na mshauri wa fedha ambaye ataweza kufuatilia masuala yako ya kifedha. Unapozingatia malengo yako ya kifedha na maendeleo, huna muda wa wasiwasi kuhusu kile ambacho kila mtu anafanya.
“Moja ya malengo yako ni lazima uwe na mfuko wa dharura,” anasema Oonnoonny wakati akizungumza kuhusu njia za kukabiliana na athari mbaya za mitandao ya kijamii. “Kuwa na fedha zilizowekwa kando katika akaunti ya ukaguzi au akiba ambayo itasaidia kulipa gharama hadi miezi sita wakati unapoteza kazi au kitu chochote kinachotokea. Hiyo pia inatafsiri [umuhimu wa] kuwa na mpango wa kifedha. Watu ambao wana mpango wa kifedha wana uwezekano mkubwa wa kulipa malipo yao ya mikopo au kutokuwa na mikopo kabisa.
Anaongeza, “Wakati mwingine unashindana na wazo la kuweka ziada [fedha] kuelekea deni la mkopo wa wanafunzi au kwenda likizo. Kuwa na malengo yako mbele na katikati ni ufunguo kwa watu wa rika”
Mitandao ya kijamii inaweza kuwa na ushawishi mkubwa katika tabia yako ya matumizi, lakini sio lazima ufunge akaunti zako zote ili kuweza kudhibiti hali yako ya kifedha. muda mwingine unachohitaji ni mpango wa kifedha na mshauri ambaye atasaidia kukupa ushauri kwenye mambo yanayohusu thamani yako na ya kifedha.
Imeandikwa na Charlene Rhinehart na kutafsiriwa na Leah Nyudike.