Home FEDHA Shein amwaga sifa Wizara ya Fedha

Shein amwaga sifa Wizara ya Fedha

0 comment 52 views

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amesema Zanzibar imekuwa ikifanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato hali ambayo imesaidia uchumi wa visiwa hivyo kuendelea kuimarika. Dk. Shein amesema hayo Ikulu Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati ikiwasilisha utekelezaji wa Mpango Kazi wa mwaka 2017/2018 na Mpango Kazi wa Utekelezaji kwa mwaka 2018/2019.

Dk. Shein ametoa pongezi kwa viongozi wa wizara hiyo pamoja na watendaji wake wote kwa kazi kubwa wanayofanya katika ukusanyaji wa mapato na kueleza matumaini yake makubwa aliyonayo kwa wizara hiyo.

Mbali na hayo, Rais Shein pia amesisitiza kuhusu umuhimu wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kutoa taarifa kwa wananchi pindi changamoto zinapojitokeza katika utoaji wa huduma zake za fedha.

Dk. Shein ametoa wito kwa Wizara ya Fedha na Mipango kuwa wazi na wananchi na kutonyamaza kimya kwani kuna kila sababu ya wananchi kufahamu mafanikio hayo pamoja na mikakati iliyowekwa na serikali kuhakikisha mapato yanaimarika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter