Home FEDHA Shein asifia sekta ya utalii Zanzibar

Shein asifia sekta ya utalii Zanzibar

0 comment 189 views
Na Mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema idadi ya wageni wanaotembelea visiwa hivyo inazidi kuongezeka kutokana na amani na utulivu unaoendelea visiwani humo. Shein ameyasema hayo baada ya kuweka jiwe la msingi katika Chuo cha Utalii kilichopo Mahurubi Unguja.

Shein ambaye anaendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwenye mikoa yote ya Unguja na Pemba amesema sekta ya utalii inachangia mapato ya serikali kwa asilimia 80 na inachangia pato la uchumi wa nchi kwa asilimia 27. Ameongeza kuwa sekta hiyo bado inahitaji kuboreshwa ili serikali ya Zanzibar ifikie malengo makubwa kiuchumi kwa kupitia vyanzo vyake vya ndani vya mapato.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud wakati anasoma taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo, amesema mkoa huo unaendelea kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na mpaka sasa kesi 361 zimeripotewa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter