Home FEDHA Tanzania yaishukuru IMF

Tanzania yaishukuru IMF

0 comment 97 views

Tanzania imelishukuru Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo kupitia misaada na mikopo nafuu inayoipatia kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.

Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba ametoa shukrani hizo Jijini Dodoma, wakati akifungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka IMF iliyowasili nchini kufanya Tathimini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF).

Program hiyo inahusika na upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na Awamu ya kwanza ya Programu ya Resilient and Sustainable Fund (RSF) ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Nchemba ameeleza kuwa inatekeleza Program ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Programu hiyo baada ya kukidhi vigezo kufuatia uongozi bora wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa masuala ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

‘‘Baada ya kutekeleza kwa mafanikio programu nyingine zilizopita ikiwepo ile ya Dirisha la Dharura ambapo tulipata fedha za kukabiliana na athari za UVIKO-19 (Rapid Credit Facility- (RCF)), na huu wa ECF unalolenga kufufua na kuimarisha uchumi, Tanzania imetimiza sifa ya kutekeleza program ya RSF ambapo tutapata fedha za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kutoka IMF,’’ amesema Dkt. Nchemba.

Amefafanua kuwa Timu za Wataalam wa pande hizo mbili zitakutana na kujadiliana zaidi kuhusu utekelezaji wa Program hizo na masuala yatakayokubalika wakati wa tathimini yatawasilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya IMF kwa ajili ya uidhinishwaji na kupata fedha.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter