Home FEDHA Waombaji wa Mikopo elimu ya juu kuhakikiwa na RITA

Waombaji wa Mikopo elimu ya juu kuhakikiwa na RITA

0 comment 76 views
Na Mwandishi wetu

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ambayo kisheria ndio taasisi pekee yenye mamlaka ya kudhibitisha taarifa na nyaraka zozote kisheria inatarajia kuanza uhakiki wa wanafunzi wa elimu ya juu kama kigezo kimojawapo cha kuomba mkopo kuanzia mwaka huu wa kimasoma 2017/2018.

RITA wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na Bodi ya mikopo (HESLB) kila mwaka kuhakiki nyaraka za wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu nchini.

Mwaka huu, wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo wanatakiwa kuhakiki vyeti vyao vya kuzaliwa na vifo katika makao makuu ya RITA au ofisi za wilaya ambazo ziliwapatia vyeti hivyo.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Kalomba Hudson ameshauri wanafunzi kufanya usajili huu mapema ili kuepukana na msongamano ofisini hapo. Wakati huo pia, Bodi ya Mikopo Tanzania (HESLB) itaendelea kupokea maombi ya mkopo hadi Septemba 4 mwaka huu.

Mwaka 2016/2017 bajeti ya Sh bilioni 340 ilitengwa kama mikopo kwa wanafunzi takribani 90,000. Baada ya bunge la bajeti mwaka huu 2017/2018, serikali iliongeza kiwango hicho hadi kufikia Sh bilioni 473 na kulenga wanufaika kuwa hadi wanafunzi 124,358.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter