• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Monday, January 30, 2023
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Waziri wa Fedha:Marekebisho Ya Sheria Ya Takwimu Hayazuii Kufanya Tafiti

Patricia Richard by Patricia Richard
October 13, 2018
in FEDHA
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

Share on FacebookShare on Twitter

Na. WFM Mjini Bali Indonesia

Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2018,  hayawazuii wadau wa takwimu kutoa takwimu kwa ajili ya matumizi yao bali marekebisho hayo yanaweka misingi ya kuzingatiwa wakati wa utoaji wa takwimu hizo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.  Philip Isdor Mpango, alipofanya mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha (IMF) anayewakilisha Tanzania na nchi nyingine (Africa Group 1 Constituency), Bw. Maxwell Mkwezalamba, katika Mikutano ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Bali Indonesia.

Dkt. Mpango amesema kuwa lengo la marekebisho ya sheria hiyo ni kurahisisha ufanyaji wa tafiti na utoaji wa matokeo ya tafiti na sio kuwabana wadau katika ukusanyaji wa taarifa za kitakwimu au kuzuia mijadala ya  uchambuzi wa kisera wa matokeo ya takwimu rasmi.

“Tumekubaliana kutumia fursa ya kuboresha Kanuni za Takwimu kwa ajili ya kuweka mazingira ya utekelezaji  mzuri wa vipengele vya sheria vilivyorekebishwa kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuelewa lengo la marekebisho hayo”, alieleza Dkt. Mpango.

Marekebisho hayo ya kanuni za takwimu yatawezesha utekelezaji mzuri wa vifungu vya sheria vilivyorekebishwa ambapo ametoa wito kwa wadau kushiriki katika mchakato wa marekebisho hayo.

ADVERTISEMENT

Aidha, Waziri  alieleza kuwa mwezi Novemba mwaka huu Serikali itakutana na wadau wa maendeleo, ili kutoa fursa kwa wadau hao kuelewa kwa kina dhumuni la Serikali kufanya marekebisho yaliyofanyika na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwezi Septemba 2018.

Vilevile, Waziri Mpango, alimueleza Mkurugenzi Mtendaji wa IMF kuwa marekebisho makubwa ya kiuchumi ambayo yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano yameambatana na mabadiliko ya sheria mbalimbali hususan  sheria za madini kwa lengo la kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi lakini pia wawekezaji wanaowekeza fedha zao nchini.

Aidha, alisema kuwa Bw. Kwezilamba, ni mwakilishi wa Tanzania kwenye Bodi ya Magavana wa IMF, hivyo ni muhimu aelewe maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanayofanyika nchini Tanzania ili aweze kueleza uhalisia kwenye mikutano ya Bodi hiyo.

Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, alisema kuwa BoT imeendelea kuboresha Sera ya Fedha ya Mwaka 2017 ili kutatua changamoto za Sekta ya Fedha zinazoibuka zikiwemo za uhaba wa mikopo hasa katika Sekta binafsi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha (IMF) anaeiwakilisha Tanzania, Bw. Maxwell Mkwezelamba, aliipongeza Tanzania kwa hatua mbalimbali za maendeleo ya uchumi kwa kuwa imeendelea kuwa nchi inayopiga hatua kubwa ya maendeleo na kuwa mfano katika nchi za Afrika.

Ameishauri Tanzania kutumia ofisi yake ili Washirika wa Maendeleo waelewe dhumuni la marekebisho ya kiuchumi yanayoenda sambamba na maboresho ya sheria mbalimbali  ili  maendeleo hayo yawe endelevu.

Vilevile Dkt. Mpango, alifanya mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB) anayewakilisha Tanzania na nchi nyingine (Africa Group 1 Constituency),  Bw. Andrew Bvumbe, wakati wa mikutano ya mwaka ya  WB na IMF inayofanyika mjini Bali Indonesia na kupongeza ushirikiano wa kimaendeleo na taasisi hizo.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikali

Wizara ya Fedha na Mipango

Mjini Bali, Indonesia

 

Tags: fedhaIMFPhilip MpangosheriatakwimuWB
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Mamlaka za mikoa zitangaze fursa za uwekezaji kuchangia uchumi wa viwanda

Discussion about this post

Habari Mpya

Mohammed Dewji (Mo Dewji). Picha|Mtandao

Watieni nguvu wawekezaji: Makalla

January 30, 2023

Vijana Tanzania kupatiwa eka 10 kulima

January 30, 2023

Poland kuisaidia Tanzania kuweka mifumo ya kodi kidigitali

January 26, 2023

Kamati ya bunge yahimiza uwekezaji maeneo ya hifadhi

January 21, 2023

Serikali kuanzisha mnada wa chai

January 20, 2023

Tumieni bandari ya Dar es Salaam: Makalla

January 19, 2023

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Mohammed Dewji (Mo Dewji). Picha|Mtandao

Watieni nguvu wawekezaji: Makalla

by Pesatu Reporter
January 30, 2023
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amewasihi mashabiki wa Simba wamtie nguvu Mwekezaji Mohammed Dewji (Mo Dewji) kwa...

Vijana Tanzania kupatiwa eka 10 kulima

by Pesatu Reporter
January 30, 2023
0

Rais Samia amesema Serikali imetenga hadi eka 10 kwa kila kijana mwenye sifa za kufanya kilimo nchini Tanzania ili kuiwezesha...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In