Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIFEDHA Fedha za miradi ambazo hazijatumika hurudi Mfuko Mkuu wa Serikali

Fedha za miradi ambazo hazijatumika hurudi Mfuko Mkuu wa Serikali

0 comments 149 views

Serikali imesema kuwa fedha ambazo hazijatumika hadi mwisho wa mwaka hurudi Mfuko Mkuu wa Serikali ikiwa ni utaratibu wa kusimamia uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya fedha zilizotengwa katika bajeti.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tandahimba Katani Ahmad Katani, aliyetaka kujua lini Serikali itarejesha fedha za miradi zilizochukuliwa na Hazina.

Dkt. Nchemba, alifafanua kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 29 cha Sheria ya Bajeti SURA 439, fedha ambazo hazijatumika hadi mwisho wa mwaka zinakoma matumizi yake na kurudishwa Mfuko Mkuu wa Serikali.

Aliongeza kuwa iwapo kuna miradi au shughuli ambazo hazijakamilika, Fungu husika linatakiwa kutenga bajeti na kuwasilisha maombi kwa kuambatisha hati za madai au nyaraka za utekelezaji wa miradi hiyo.

Dkt. Nchemba alisema kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa miradi yote inatekelezwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!