• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Monday, January 30, 2023
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Fuga samaki kisasa

Patricia Richard by Patricia Richard
May 16, 2018
in UJASIRIAMALI
0
Share on FacebookShare on Twitter

Endapo watanzania watabadilika na kutumia mbinu za kisasa za kilimo na ufugaji ikiwemo ufugaji wa samaki basi wanaweza kujiingizia kipato na kupiga hatua kimaisha. Ufugaji  huu ni nafasi nzuri kwa wadau kufanya kilimo mseto na kutumia ardhi kwa mazao na mifugo hivyo kupata faida zaidi.

Ufugaji huu unachohitaji zaidi ni ardhi ya kutengezea bwawa. Upatikanaji wa maji ya uhakika pia ni jambo la msingi. Kwa mfugaji mdogo mbinu nyingine za kuhifadhi maji kama kutumia debe inaweza kutumika. Ufugaji huu unahitaji umakini mkubwa hivyo inashauriwa mfugaji kuwa na ufahamu kuhusiana na samaki. Muda gani wa kuwalisha, usafi wa bwawa na kipimo ambacho maji yanatakiwa kuwepo muda wote.

Baada ya hili kukamilika mfugaji anaweza kuamua ni aina gani ya samaki anataka. Zipo aina mbalimbali za samaki ambao wanaweza kufugwa nyumbani. Sato na Kambale ndio wanaofugwa kwa wingi. Hakikisha kuwa kila mita moja ya mraba samaki hawazidi 8. Si vizuri kuwajaza wengi katika eneo dogo kwani watakosa hewa.

Ni muhimu kuwa makini wakati wa kununua vifaranga vya samaki. Ni vizuri kujiridhisha kuwa mbegu unazonunua zipo katika hali nzuri. Mbegu ya sato hupatikana kwa bei ya rejareja kuanzia 300 Sh huku kambale ikiwa ni 500 Sh kwa kifaranga kimoja. Tanzania Fisheries Research Institute (TAFIRI) ya Nyegezi Mwanza ni moja kati ya sehemu ambazo vifaranga hivi hupatikana.

ADVERTISEMENT

Kwenye chakula, samaki hula kulingana na uzito wao. Wakiwa wadogo wanakula asilimia 5 ya uzito wao na kadri wanavyoongezeka hufikia hadi asilimia 3. Ni muhimu kufahamu kuwa kuna aina mbili za chakula cha samaki.

Cha kwanza ni chakula cha asili kinachotokana na mbolea ambacho huchanganywa na maji na kukaa kwa angalau siku 21. Kufanya hivi kunawatengenezea samaki mazingira mazuri ya kujitafutia chakula chao wenyewe. Mara nyingi kinakuwa katika mfumo wa mimea au vijidudu.

Aina ya pili ni chakula ambacho mfugaji hupaswa kuwalisha samaki. Ni muhimu kuwa na muda maalum wa kuwapatia chakula ambao haubadiliki mara kwa mara ili kujenga mazoea na kuwa na rekodi ya muda gani samaki wanakula.

Wafugaji wa samaki wana haja ya kuwa watunzaji na wachukuaji takwimu. Rekodi za uzalishaji na mauzo yao zitasaidia kwenye uombaji wa mikopo kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za kiserikali. Ufugaji huu unaashiria matumaini makubwa. Tukiendelea hivi, hata serikali nayo itasukumwa kuweka nguvu nyingi zaidi katika sekta hii ya ufugaji wa kisasa.

 

 

Tags: samakiTAFIRIUfugaji wa kisasa
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post

Emirates iliyotua ghafla Dar yaleta baraka

Discussion about this post

Habari Mpya

Poland kuisaidia Tanzania kuweka mifumo ya kodi kidigitali

January 26, 2023

Kamati ya bunge yahimiza uwekezaji maeneo ya hifadhi

January 21, 2023

Serikali kuanzisha mnada wa chai

January 20, 2023

Tumieni bandari ya Dar es Salaam: Makalla

January 19, 2023
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Jukwaa la Uchumi Duniani.

Sekta ya kilimo kukua kwa 10% 2030: Rais Samia

January 19, 2023

Ndege tano kuwasili mwaka huu

January 17, 2023

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Poland kuisaidia Tanzania kuweka mifumo ya kodi kidigitali

by Pesatu Reporter
January 26, 2023
0

Poland imeahidi kuisadia Tanzania kuimarisha mifumo ya kodi kwa njia ya kidigitali ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya...

Kamati ya bunge yahimiza uwekezaji maeneo ya hifadhi

by Pesatu Reporter
January 21, 2023
0

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeishauri Wizara ya Maliasili na Utalii iendelee kuzifanyia maboresho kanuni...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In