Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Serikali kugawa maeneo kwa vijana

Serikali kugawa maeneo kwa vijana

0 comment 32 views

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Anthony Mavunde amesema serikali imepanga kutenga maeneo maalum kwa ajili ya vijana kufanya shughuli za kijasiriamali ikiwa ni njia mojawapo ya kuwapa nafasi ya kujiajiri na kupunguza changamoto ya ajira,

Mavunde amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizindua maonyesho ya wanafunzi wa chuo kikuu cha St. Joseph na kutoa agizo kwa manispaa zote nchini kutenga maeneo hayo. Naibu Waziri huyo amedai mpango huu unatekelezwa baada ya taarifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kuonyesha takribani asilimia 70 ya vijana wanashinda mitaani kutokana na kutokuwa na ajira.

“Takwimu kutoka NBS baada ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonesha asilimia 70 ya vijana wanashinda vijiweni na kupiga stori na hii inatokana na wao kukosa ajira za kufanya na tunazitaka manispaa zote nchini kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya vijana kufanya shughuli zao za kimaendeleo”. Ameeleza Mavunde.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema mipango mingine ya serikali kutatua matatizo yanayowakabili vijana ni pamoja na kuyatambua makundi ya vijana, kutoa  elimu ya ajira na kuwarasimisha vijana wajiunge katika vikundi (Saccos) ili mikopo iwafikie kwa urahisi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter