Kutokana na kukua kwa teknolojia, vijana wa Kitanzania wametakiwa kutumia fursa za kidigitali ili kuweza kukuza ubunifu na ujasiriamali na kupata masoko ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Venture, Jumanne Mtambalike ametoa wito huo kwa vijana katika Kongamano la ubunifu, teknolojia na ujasiriamali lililoandaliwa Sahara Ventures kwa kushirikana na wadau wengine wakiwemo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH).
Mtambalike amesema “tunafungua fursa mbalimbali kwa vijana kwenye maeneo ya ubunifu teknolojia pamoja na ujasiriamali”.
Ameeleza kuwa kongamano hilo ambalo ni la wiki moja wanategemea vijana watajifunza mambo mengi zaidi ambapo kuna matamasha na mada mbalimbali yatafanyika.
Amebainisha kuwa wanashirikiana na COSTECH, kwa sababu wanawaunga mkono vijana katika kukuza ubunifu wao na wataendelea kufanya hivyo hata kwa vijana wa mikoani kufanya ubunifu na teknolojia kuendelea.