Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Wajasiriamali Zanzibar kuunganishwa nje

Wajasiriamali Zanzibar kuunganishwa nje

0 comment 39 views

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali ameahidi kuwa serikali itawaunganisha wajasiriamali kutoka taasisi ya “Mwanamke Chakarika” na taasisi nyingine za nje ili wajasiriamali hao waweze kujifunza maarifa mapya na kuwa wabunifu zaidi katika biashara na kukidhi viwango vinavyokubalika kimataifa. Balozi Ali amesisitiza kuwa serikali kupitia wizara hiyo itahakikisha bidhaa kutoka Zanzibar zinavuta soko la ndani na kimataifa na kutoa wito kwa wajasiriamali kutumia vizuri matamasha na maonyesho ya kibiashara kujitangaza kwani ni njia mojawapo ya kuwafikia wateja.

“Masoko yanatafutwa kwa njia na mbinu mbalimbali, Wizara yangu imepata jengo ndani ya Mji Mkongwe ambalo tutalitumia kuonyesha bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wetu ili kukuza uwezo wao wa uzalishaji na kuwapatia soko la bidhaa zao”. Amesema Waziri huyo.

Vilevile, Balozi Ali ametumia fursa hiyo kuwashauri vijana kubadilika na kuanza kutumia maarifa na ujuzi walionao kujiajiri katika sekta mbalimbali ili kupambana na changamoto ya ajira badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini.

Kwa upande wake, Katibu wa taasisi ya Mwanamke Chakarika amesema wameandaa kongamano hilo kwa lengo la kutoa hamasa kwa wanawake na vijana kujiajiri wenyewe badala ya kupoteza muda wakisubiri ajira ambazo hutoka kwa uchache.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter