Home KILIMO Dk. Shein apongeza Wizara ya Kilimo

Dk. Shein apongeza Wizara ya Kilimo

0 comment 33 views
Na Mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amepongeza Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Kusini Pemba hadi kubaini na kurejesha serikalini mashamba ambayo yalikuwa yanamilikiwa na serikali hapo mwanzo huku akiwaonya watu wote wanaoendelea kuyaficha mashamba hayo kuwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao pindi watakapogundulika.

Dk. Shein ameagiza taratibu na sheria kuchukuliwa bila kujali cheo au wadhifa wa mtu. Pia amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kutojiingiza kwenye utetezi wa wafanyabiashara ambao walitakiwa kulipa zao kama alivyoagiza lakini wamekiuka kufanaya hivyo, jambo ambalo linakosesha serikali mapato.

Rais huyo ambaye anahitimisha ziara yake ya kuangalia miradi ya maendeleo visiwani humo pia ameagiza Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kufanya mkutano maalum na viongozi wa mikoa na wilaya zote ili kujadili na kupeana majukumu ya utekelezaji wa utalii kwa wote.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter