Home KILIMOKILIMO BIASHARA Kibano wauza mbegu, mbolea feki nchini chanja

Kibano wauza mbegu, mbolea feki nchini chanja

0 comments 87 views

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali iko mbioni kutunga Sheria itakayowabana wauzaji wa mbegu, viuatilifu na mbolea feki ili waweze kuhukumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi kuanzia msimu ujao wa kilimo.

Waziri Bashe amesema hayo akiwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Taifa wa Wadau wa Tasnia ya Mbegu Mei 15, 2025 uliofanyika katika Ukumbi wa Midland Hotel, jijini Dodoma.

“Sheria iliyopo sasa haina meno ya kuwabana wauzaji wanaobainika kuuza mbegu feki kwa kuwa faini wanazotozwa ni ndogo kuliko hasara wanayoisababisha katika jamii”, amesema Waziri Bashe.

Ameongeza kuwa mtu anayewauzia wakulima mbegu feki anatakiwa kuhukumiwa lakini sheria iliyopo sasa inawatoza wauzaji hao faini kati ya Shilingi 500,000/=hadi shilingi 1,000,000/ ambayo hailingani na makosa waliyoyafanya.

Aidha, Waziri Bashe ametoa rai kwa wauzaji na wasambazaji wote wa mbegu nchini kuwa waaminifu na kuhakikisha wanauza na kusambaza mbegu bora na halali ambazo zina nembo ya Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ili zitumike kwa kuleta uzalishaji wenye tija kwa wakulima ili kuendana na azma ya Serikali katika Agenda 10/30.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!