• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Sunday, June 26, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Faida 4 za kutumia mabanda ya kisasa

Ni muhimu kwa wafugaji kupewa elimu zaidi kuhusu teknolojia za kisasa.

Abdul Kassim by Abdul Kassim
May 11, 2020
in BIASHARA, KILIMO UFUNDI
0
Share on FacebookShare on Twitter

Jambo moja la msingi katika ufugaji wa kuku ni mabanda ya kufugia na kutokana na ubora wake, mfugaji anaweza kupata mafanikio au hasara kwani kuku hukua na hutaga zaidi katika mazingira mazuri na salama. Siku hizi kuna mabanda ya kisasa yaliyo katika mfumo wa betri ambayo yanamrahisishia mfugaji kufuga katika hali ya usafi na salama. Wafugaji wengi ambao wanatumia mabanda hayo wamekuwa wakifurahia matokeo.

Bei zake hutegemea aina ya banda na kiasi cha kuku waliopo lakini  kwa makadirio mabanda mengi ya kuku ya kisasa ya mfumo wa betri huuzwa kati ya Sh. 450,000 (kwa ajili ya vifaranga), uwezo wake ukiwa vifaranga 400, na kwa kuku wakubwa (layers) huuzwa kwa Sh. 750,000 na uwezo wake ni kuku 96 katika banda moja.

Hizi ni faida  nne za kutumia mabanda ya kisasa katika ufugaji wa kuku hususani wa mayai:

ADVERTISEMENT

Huokoa nafasi

Kwa wafugaji wa kuku ambao wana changamoto ya nafasi kwa ajili ya kufugia wanaweza kusuluhisha changamoto hiyo kwa kutumia mfumo wa kisasa wa mabanda ya kufugia, kwani katika mabanda hayo ya kisasa huwa kunakuwa na nafasi ambayo kuku wanaweza kufugwa katika mpangilio mzuri zaidi. Kwa mfano kuna mabanda ambayo yanaweza kufuga kuku 96, kuna mabanda ambayo hukaa kama gorofa ambayo huruhusu ufugaji wa kuku 128 hadi 300 hivyo mkulima anaweza kununua banda ambalo linakidhi kiasi cha kuku anaotaka kufuga bila kuwaza kuhusu nafasi.

Ubora

Kupitia mabanda ya kisasa mfugaji hupata urahisi wa kulisha vizuri kuku na kuwatunza kwa umakini zaidi jambo ambalo hupelekea kuku kuwa na afya njema na kutaga mayai bora yaliyo katika hali ya usafi ambayo mwisho wa siku mkulima huyapata katika mfumo ambao tayari umetengenezwa katika mabanda hayo hivyo kuepuka upotevu wa muda kwa kuanza kusafisha, jambo ambalo linaweza kusababisha mayai yachelewe kuwafikia wateja kwa wakati. Kupitia mabanda haya ufugaji wa kuku wa mayai umerahisishwa na kumuwezesha mfugaji kapata bidhaa bora.

Gharama

Mabanda ya kisasa yaliyo katika mfumo wa betri yamerahisisha kazi kwa asilimia kubwa hivyo hakuna haja ya kuajiri watu wengi kwa ajili ya kuangalia kuku. Kila kitu kimeshapangwa katika mfumo huo, ikiwa ni pamoja na mpangilio wa kuku wenyewe, sehemu maalum ya kulisha na kuwawekea maji, sehemu ya mayai kupita na sehemu ya mfugaji kuchukua mayai hayo. Kazi iliyopo ni kuwamiminia chakula na maji kupitia maeneo yaliyotengwa na kuhakikisha mayai na uchafu yanatolewa kila baada ya muda ili kuku waendelee kutaga katika mazingira safi na salama.

Hupunguza magonjwa

Kutokana na kila kuku kuwa na sehemu yake si rahisi kuambukizana magonjwa. Pia mfumo maalum wa kutolea kinyesi unagfanya iwe ngumu kwa kuku kufikia kinyesi chao na kupata maambukizi mbalimbali. Vilevile ni rahisi zaidi kutambua na kuchukua hatua kwa kuku wenye magonjwa kabla hawajasambaza kwa  kuku wengine.

Aidha, ni muhimu kwa wafugaji kupewa elimu zaidi kuhusu teknolojia za kisasa zinazohusiana na ufugaji ili kuweza kunufaika na ufugaji wao bila kutumia nguvu nyingi. Watanzania wengi wameendelea kuwekeza katika sekta hii ya ufugaji hivyo ni wakati muafaka kwa serikali na wadau mbalimbali kuwaunga mkono kwa kuwapa elimu sahihi.

Abdul Kassim

Abdul Kassim

Next Post

Umuhimu wa bima kwa wafanyabiashara

Discussion about this post

Habari Mpya

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 24, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 23, 2022

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 23, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 22, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 22, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 20, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 24, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

by Pesatu Reporter
June 23, 2022
0

Mapendekezo yamepitishwa kwa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) leo 23...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In