Home KILIMO SAGCOT NA Korea kusini kuimarisha kilimo nchini

SAGCOT NA Korea kusini kuimarisha kilimo nchini

0 comment 70 views
Na Mwandishi wetu

Kituo cha Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (Sagcot) kwa kushirikiana na serikali ya Korea Kusini wamesaini makubaliano ya kukuza kilimo cha umwagiliaji ili kusaidia wakulima waliopo vijijini.

Taasisi ya Korea Rural Community Corporation (KRC), ambayo ndiyo itafanikisha makubaliano haya inakusudia kuboresha sekta mbalimbali katika kilimo zikiwemo ujenzi wa mabwawa na mifereji pamoja na kutoa elimu ya kilimo cha kisasa katika ukanda wa kusini nchini.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sagcot Geoffrey Kirenga amesema wakulima wadogo wa kanda za kusini watanufaika na mabadiliko yatayopatikana mara baada ya utekelezwaji wa mpango huu. Ameongeza kwamba kilimo cha kisasa kinahitaji teknolojia na uwezekaji mkubwa hivyo makubaliano haya yatatoa mwanga kwa wakulima wa vijijini ambao kwa sasa wanakosa fursa nyingi kwa kukosa mitaji ya kutosha.

Naye Rais wa KRC Chung Seung amesema wamejipanga kuhakikisha wakulima wanakuwa na mifereji na mabwawa ya maji katika mashamba yao ili waweze kuendesha kilimo chao kwa mwaka mzima bila kutegemea msimu, aliongeza kuwa ujio wake hapa nchini umetokana na ombi la Balozi wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter