Home KILIMO Hasunga: Serikali inafanya mengi kuboresha kilimo

Hasunga: Serikali inafanya mengi kuboresha kilimo

0 comment 15 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuboresha kilimo na kuleta mapinduzi katika sekta hiyo. Waziri Hasunga ameeleza kuwa japokuwa kilimo kinachangia takribani asilimia 30 ya pato la taifa, ukuaji wa sekta ya kilimo bado sio wa kuridhisha kutokana na changamoto zinazowakabili wakulima na wadau wengine wa sekta hiyo.

Waziri huyo amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa wadau wa asasi zinazotoa huduma ndogo za kifedha vijijini kwa wajasiriamali wadogo (TAMFI). Katika maelezo yake, Hasunga amesema Wizara ya Kilimo, Wizara za Sekta ya Kilimo (ASLMs) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ili kuboresha mazingira ya kilimo na kuchochea uzalishaji, kwani kufanya hivyo kutawezesha sekta hiyo kuwa kibiashara zaidi na hivyo kuinua kipato cha wakulima wadogo.

“Umefika wakati sasa tuhamasishe kuwa na Kilimo cha mashamba makubwa na ya kati yatakayopelekea kuzalisha kwa wingi na kwa tija”. Amesema Waziri huyo.

Wadau mbalimbali wameshiriki mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania wakiwemo maafisa wa serikali, watoa huduma za kifedha vijijini, wataalam wa fedha, wakulima na wawakilishi wa mashirika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter