Home KILIMO Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji chakula Afrika

Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji chakula Afrika

0 comment 59 views

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ina malengo ya kuwa kitovu cha uzalishaji chakula barani Afrika

Rais Dkt. Samia amesema hayo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati akizungumza na Maafisa Ugani wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika Agosti 10, 2024.

Amewataka Maafisa Ugani na Ushirika kuzidi kuwaelimisha wakulima njia bora za kilimo kwani Tanzania ili kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji chakula barani Afrika.

Dkt Samia ameeleza mchango wa kilimo kwa Pato la Taifa unachangiwa na juhudi za Maafisa Ugani kutokana na maarifa wanayowapa wakulima kwenye kuchangia utoshelevu wa chakula nchini.

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewaambia maafisa hao kuwa kutakuwa na utaratibu wa kuwapima kupitia wakulima kwa hiyo wanatakiwa waongeze juhudi katika kutekeleza majukumu yao.

Rais Dkt. Samia akizungumza na Maafisa Ugani wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika Agosti 10, 2024.

Rais Dkt. Samia ametaja sababu zinazopelekea Serikali anayoiongoza kuipa kipaumbele sekta ya kilimo kwa kuwa inagusa maisha ya idadi kubwa ya Watanzania, uhakika wa usalama wa chakula na uwepo wa fursa za ajira kwa vijana.

Kuhusu uhakika na usalama wa chakula, Rais Dkt. Samia amesema Serikali inaendelea na juhudi za kuwekeza kwenye teknolojia za kisasa na umwagiliaji ili kuwa na uhakika wa uzalishaji katika kipindi hiki ambacho Dunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi na kupelekea kutokuwa na uhakika wa uzalishaji wa chakula miongoni mwa nchi nyingi Duniani.

Aidha, Rais Dkt. Samia emeongeza kuwa uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo utawezesha vijana wengi kujiajiri na wengine kuajiriwa kwani kilimo ni biashara.

Amewapongeza Mafisa Ugani kwa kuwa wanataaluma muhimu wenye kutoa miongozo na maarifa kwa wakulima na hatimaye kuwezesha Taifa la Tanzania kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 128.

Aidha, amevitaka Vyama vya Ushirika vijiandae kujitegemea kwani ruzuku ni za mpito.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter