Home KILIMO Wanaosambaza mbegu feki waonywa

Wanaosambaza mbegu feki waonywa

0 comment 56 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ametangaza kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaouza mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali na kuwataka wafanyabiashara wote ambao wamekuwa wakijishughulisha na vitendo hivyo kuacha haraka kwani serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo. Waziri Haunga ametoa agizo hilo mkoani Morogoro ambapo mbali na hayo alitembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), taasisi ambayo ilipewa jukumu la kusajili wafanyabiashara wa mbegu na serikali.

“Serikali imepokea malalamiko mengi kwa wananchi kuhusu ubovu wa mbegu jambo ambalo limepelekea kwa kiasi kikubwa kuwa na mavuno kidogo pasina kukidhi matakwa ya wakulima wetu nchini. Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu mbegu feki jambo hili serikali haiwezi kukubaliana nalo hivyo TOSCI wanapaswa kusimamia kwa weledi ukaguzi na usajili wa mbegu bora, pia ni lazima kuwabaini wasambazaji feki wa mbegu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao”. Amesisitiza Hasunga.

Waziri Hasunga amesema wizara ya kilimo imebeba jukumu la kuhakikisha sekta ya kilimo hapa nchini inaimarika kwa kuzingatia usimamizi madhubuti wa sera, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali hivyo uwepo wa malalamiko ya wananchi kuhusu mbegu feki ni ishara kuwa taasisi zilizobeba jukumu hilo hazitekelezi kazi zake kwa ufasaha.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter