Home LifestyleTravel Hizi hapa nchi 71 raia wake kuingia Tanzania bila VIZA

Hizi hapa nchi 71 raia wake kuingia Tanzania bila VIZA

0 comments 100 views

Serikali imeingia makubaliano na nchi mbalimbali ili kurahisisha utaratibu wa viza ambapo raia wa nchi 71 hawahitaji viza wanapoingia nchini.

kwa sasa watalii kutoka mataifa mengi zaidi duniani wanaruhusiwa kupata visa wanapowasili (visa on arrival) kwenye viwanja vya ndege vya kimataifa kama Julius Nyerere (Dar es Salaam), Kilimanjaro na Zanzibar.

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa maliasili na utalii Dunstan Kitandula alipokuwa akijibu swali la Dkt. Pius Stephen Chaya aliyetaka kujua ni jitihada gani zimefanyika kurahisisha upatikanaji wa VISA kwa watalii wenye uraia tofauti wanaokuja nchini kwa mwitikio wa Tanzania the Royal Tour.

Naibu Waziri wa maliasili na utalii Dunstan Kitandula

Aidha Kitandula aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha utaratibu wa utoaji wa viza nchini ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani. Mathalan, Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji imeanzisha mfumo wa maombi ya viza kwa njia ya mtandao (e-Visa) unaowawezesha watalii kuomba viza popote walipo duniani bila kulazimika kufika ubalozini.

“Halikadhalika, Serikali imeboresha Kanuni za Uhamiaji za mwaka 2023 (GN 428) ambapo kwa sasa watalii wanaotumia Visitors Pass wanaruhusiwa kutembelea Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kurejea Tanzania bila hitaji la kuomba upya pasi ya kuingia nchini” alisema Kitandula

Suala la visa lina uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii imeimarisha ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Ndani, hususan Idara ya Uhamiaji, katika nyanja mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa takwimu za watalii na kuwa na mikakati ya pamoja ya kuvutia watalii na fursa za uwekezaji.

Aidha, siku za hivi karibuni, Wizara kupitia Chuo cha Taifa cha Utalii imetoa mafunzo ya Huduma kwa Wateja na Ukarimu kwa Maafisa wa Jeshi la Uhamiaji ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa wageni wanaoingia nchini, ikiwemo watalii.

1. Antigua & Barbuda
2. Anguilla
3. Ashmore & Certie Island
4. Bahamas
5. Barbados
6. Bermuda
7. Belize
8. Brunei
9. British Virgin Island
10. British Indian Ocean Territory
11. Botswana
12. Burundi
13. Cyprus
14. Cayman Island
15. Channel Island
16. Cocoas Island
17. Cook Island
18. Christmas Island
19. Democratic Republic of Congo (DRC)
20. Dominica (Commonwealth of Dominica)
21. Falkland Island
22. Gambia
23. Ghana
24. Gibraltar
25. Grenada
26. Guernsey
27. Guyana
28. Heard Island
29. Hong Kong, China
30. Isle of man
31. Jamaica
32. Jersey
33. Kenya
34. Kiribati
35. Lesotho
36. Malawi
37. Montserrat
38. Malaysia
39. Madagascar
40. Malta
41. Mauritius
42. Macao, China
43. Mozambique
44. Nauru
45. Naue Island
46. Norfolk Island
47. Namibia
48. Papua new Guinea
49. Rwanda
50. Romania
51. Ross Dependency
52. Samoa
53. Seychelles
54. Singapore
55. Swaziland
56. Solomon Island
57. South African Republic
58. South Sudan
59. St. Kitts&Navis
60. St. Lucia
61. St. Vicent
62. St. Helana
63. Trinidad & Tobago
64. Turks & Caicos
65. Tokelan
66. Tonga
67. Tuvalu
68. Vanuatu
69. Uganda
70. Zambia
71. Zimbabwe

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!