Home KILIMO Nguzo za umeme kulipiwa ushuru

Nguzo za umeme kulipiwa ushuru

0 comment 109 views

Waziri mkuu wa Tanzania,mheshimiwa Kassim Majaliwa ameagiza kampuni zote zinazovuna na kusambaza nguzo za umeme nchini kulipa ushuru kwa halmashauri husika zinapotoka nguzo hizo kwa mujibu wa sheria ya fedha za serikali za mitaa.

Waziri mkuu amesema hayo kufuatia kubaini kukosekana kwa umeme katika baadhi ya vijiji mkoani Ruvuma kulikosababishwa na ukosekanaji wa nguzo zilizozuiwa na baadhi ya halmashauri kutokana na kutokulipiwa ushuru na kampuni ya New forest inayohusika kusambaza nguzo hizo.

Uamuzi huo unakuja baada ya kikao baina ya waziri huyo na waziri wa nishati,Medard Kalemani,Waziri wa Tamisemi,Selemani Jaffo na mkuu wa mkoa wa Iringa,Ally hapi ambao aliwataka wamueleze kwa kina chanzo cha tatizo hilo hasa katika baadhi ya wilaya kama mufindi.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu inaeleza kuwa waziri huyo ameagiza kulipwa kwa ushuru huo wa 5% kama isemavyo sheria baada ya kubaini ukiukwaji mkuu wa sheria unaofanywa na kampuni ya new forest ambayo imepewa jukumu la kimkataba na tanesco kusambaza nguzo hizo hivyo kulipikiza madeni zaidi ya bilioni 2.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter