Home Uncategorized TIGO yatumia milioni 18 kumaliza tatizo la maji

TIGO yatumia milioni 18 kumaliza tatizo la maji

0 comment 109 views

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya ziwa Ally Maswanya

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imejenga kisima cha maji chenye thamani ya Sh.18 milioni katika kijiji cha Usongelani wilayani Urambo mkoa wa Tabora. Katika sherehe ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Tigo kanda ya ziwa Ally Maswanya amesema kisima hicho kitasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi wa eneo hilo.

Maswanya ameongeza kuwa Kampuni ya Tigo inajitahidi kuboresha maisha ya jamii sio tu katika huduma za mawasiliano bali katika masuala ya afya na ustawi wa wananchi. Msaada huo utanufaisha wananchi zaidi ya 187,000 huku mkurugenzi huyo akidai kampuni hiyo inalenga kuchimba vizima zaidi katika maeneo yaliyo na uhitaji mkubwa.

Katika sherehe hizo pia, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameshukuru kampuni ya Tigo kwa msaada wa kujenga kisima hicho akisema kitasaidia kuimarisha afya kwa kiasi kikubwa na pia kusaidia ukuaji wa wananchi kiuchumi na kijamii.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter