Home VIWANDAMIUNDOMBINU Sijapendezwa na vibanda nilivyoviona bandarini: Rais Samia

Sijapendezwa na vibanda nilivyoviona bandarini: Rais Samia

0 comment 35 views

Rais Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya upanuzi wa bandari ndogo ya Ujiji na Kibirizi mkoani Kigoma.

Samia ameweka jiwe hilo la msingi Oktoba 18, 2022 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoani humo ambapo tayari amefanya shughuli mbalimbali ikiwemo uzimaji wa majenereta baada ya Kigoma kuunganishwa na gridi ya Taifa.

Rais Samia amesema wakati akiingia bandari ya Kibirizi hakufurahishwa na sura aliyoiona nje ikiwemo barabara na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo.

Ameutaka uongozi wa mkoa huo kushirikiana na wataalamu kuandaa ramani itakayopendezesha eneo la kuingia bandarini ikiwemo kujenga miundombinu mipya ya wafanyabiashara.

Amesema tayari ameteta na Waziri wa Ujenzi ili waisaidie Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) kujenga barabara inayoingia bandarini hapo.

“Lakini pia sikupendezwa na vibanda nilivyoviona, kwa maana hiyo kuna haja ya mwongozo wa mkoa na wilaya hii, kuliangalia hilo eneo, kushirikiana na wataalamu kupata ramani itakayopendezesha eneo hili la biashara ya kuingia bandarini.

“Ombi langu kwenu wafanyabiashara wa eneo hili, tukubaliane na yale yakayokuja kufanyika kwa sababu maendeleo ni kuharibu kwanza, lazima tubomoe vibanda vilivyopo, tufanye ramani mpya halafu soko litakalokubaliwa lijengwe, halafu wale walioondoshwa warudishwe,” amesema Samia.

Amewataka wakae na umoja wao wa wafanyabiashara wakubaliane jinsi eneo hilo litavyotengenezwa ili mtu atakapotoka bandarini akute wafanyabiashara wakiwa katika maeneo mazuri na wanafanya biashara nzuri wakati akienda kutafuta fedha za kujenga eneo hilo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter