Home VIWANDANISHATI Petroli, dizeli zashuka, mafuta ya taa yapanda

Petroli, dizeli zashuka, mafuta ya taa yapanda

0 comment 109 views

Bei ya mafuta ya petrol na dizeli zimeshuka kutoka Tsh 3,281 hadi 3,274 kwa lita ya petroli na Tsh 3,448 hadi 3,374 kwa lita ya dizeli kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za bidhaa za mafuta zinazoanza kutumika Novemba 01,2023.
Bei hizo zimeshuka kwa viwango tofauti tofauti kwa mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Mtwara.

Kwa mkoa wa Tanga petroli itauzwa kwa Tsh 3,320 ikilinganisha na 3,353 kwa mwezi uliopita huku dizeli ikiwa ni Tsh 3,510 ukilinganisha na 3,520 kwa mwezi Oktoba.

Kwa mkoa wa Mtwara petroli itauzwa kwa Tsh 3,347 ikilinganisha na 3,353 kwa mwezi Oktoba huku dizeli ikiwa Tsh 3,546 ambapo mwezi uliopta iliuzwa 5,520.

“Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Oktoba 2023 yanatokana na kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 5.68 na gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 13 kwa petrol na asilimia 25 kwa dizeli.
Pia uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani (OPEC+) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo nchi ya Urusi imewekewa,” inaeleza taarifa hiyo.

Taarifa ya Ewura inaonesha kupanda kwa bei ya mafuta ya taa kutoka 3,016 hadi 3,495.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter