Home VIWANDANISHATI Umeme kufika kila kijiji

Umeme kufika kila kijiji

0 comment 32 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema kupitia mradi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya tatu, hakuna kijiji kitakachoachwa pasipo kuunganishiwa umeme nchini kwani serikali imetenga Shilingi trilioni moja maalum kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa na nishati hiyo, wakati huo huo zoezi la uwekaji wa umeme katika vijiji zaidi ya 13,400 likiendelea.

Hasunga amesema hayo katika mikutano yake katika kijiji cha Igale na Iyula A akiwa katika ziara ya kikazi kama Mbunge wa jimbo la Vwawa mkoani Songwe. Waziri huyo amesema upatikanaji umeme jimboni kwake utasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kuchochea maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Mbali na hayo, Waziri huyo amewataka wananchi jimboni humo kutumia fursa mbalimbali zinazotokana na utekelezaji wa miradi katika sekta ya gesi na mafuta ili kuongeza kipato na kufanikisha nchi kutimiza malengo yake ya kufikia uchumi wa kati.

Kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya gharama kubwa za pembejeo za kilimo, Waziri Hasunga amesema wizara yake inafanya mchakato kuhakikisha mbolea zinapatikana kwa wakati muafaka ili wakulima waweze kunufaika na pembejeo hizo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter