Home VIWANDAUZALISHAJI Kigoma yatajwa kwenye orodha ya mikoa inayolegalega utekelezaji miradi

Kigoma yatajwa kwenye orodha ya mikoa inayolegalega utekelezaji miradi

0 comment 66 views

Mkoa wa Kigoma imetajwa kuwa miongoni mwa mikoa inayolegalega katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa, ameutaja mkoa huo Agosti 12, 2024 wakati wa ziara yake mkoani Kigoma alipokutana na kuzungumza na watumishi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo pamoja na watendaji wa taasisi mbalimbali za umma ngazi ya mkoa na wilaya.

Baadhi ya watumishi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma pamoja na watendaji wa taasisi mbalimbali za umma ngazi ya mkoa na wilaya.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia OR – TAMISEMI analeta fedha za kutosha kutekeleza miradi yote nchi nzima, sisi watendaji hatuna namna yoyote ile tunayoweza kusema kwa nini tunalegalega katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo” amesema Waziri Mchengerwa.

Amewataka watendaji kuongeza juhudu katika kutekeleza miradi mikubwa ya serikali na utoaji wa huduma kwa jamii.

Waziri Mchengerwa amesema wananchi wana kiu kubwa ya maendeleo wakitamani kuona miradi inayotekelezwa katika maeneo yao inakamilika kwa wakati hivyo watendaji hawana kisingizio chochote cha kuchelewesha miradi hiyo.

Ameongeza kuwa Ofisi yake haitamvumilia mtendaji yeyote anayelegalega katika kipindi chake akisisitiza uwajibikaji kwa jamii na utatuzi wa kero za wananchi kuwa kipaumbele namba moja kwa watendaji wake.

“Mimi na Wakurugenzi tumekubaliana miradi yote inayohiusu OR- TAMISEMI iwe imekamilika kufikia Desemba 30, 2024, na kwenye hili Wakuu wa Wilaya simamieni, fuatilieni kwa ukaribu miradi hii ni ya kwenu, sasa tukisikia miradi haijakamilika maana yake na nyinyi mnahusika moja kwa moja tusiwaonee wakurugenzi peke yake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa.

Kuanzia sasa nataka niwaone mkiwa bega kwa bega kukagua kila mradi uliopo kwenye wilaya zenu na mtushauri maana taarifa zenu zitatusaidia sana kufanya maboresho kuliko taarifa tukizipata kienyeji na kupitia kwenye vyombo vya habari, amesema Waziri Mchengerwa”.

Aidha, amewataka watendaji katika mamlaka yake kuwa msatari wa mbele kubainisha changamoto za maeneo wanayo yahudumia ili kuweka urahisi kwa viongozi wenye mamlaka kuzitafutia ufumbuzi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter