Home VIWANDAUZALISHAJI Tanzania kunufaika na teknolojia kuzalisha mbolea kutoka Cuba

Tanzania kunufaika na teknolojia kuzalisha mbolea kutoka Cuba

0 comments 111 views

Katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) limesaini mikataba miwili ya ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba ili kuzalisha mbolea hai.

Hafla hiyo imefanyika Mei 04, 2025 jijini Dar es Salaam ambapo mbolea hiyo itayosambazwa na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na kuimarisha teknolojia ya kisasa.

Tukio hilo limehudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole ambaye ameratibu na kuhamasisha uwekezaji huo wa kimkakati hapa nchini.

Balozi Polepole amesema kuwa hatua hii imefikiwa kutokana na dhamira ya nchi ya Tanzania na nchi ya Cuba kuendeleza ustawi wa wananchi wake kupitia uhawilishaji wa teknolojia na maarifa.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo Tanzania, Dkt. Nicolaus Shombe ameeleza kuwa Tanzania inakwenda kunufaika na teknolojia ya uzalishaji wa mbolea hai na viuatilifu.

“Ushirikiano huu unatokana na mahusiano yaliyojengwa na waasisi wetu baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere na kiongozi Mstaafu wa Cuba Fidel Castro,” amesema Dkt. Shombe.

Amesema kusainiwa kwa mikataba hiyo sekta ya kilimo inakwenda kunufaika kwa kupata teknolojia ya kuzalisha mbolea salama isiyo madhara kwa binadamu na mazingira

Ameongeza kuwa hiyo ni fursa kwa Watanzania katika Sekta ya Ajira, kulinda afya za Watanzania, kuimarisha uchumi kwa kuzalisha mbolea nchini ambayo pia ni rafiki kwa mazingira.

Julio Gonzalez ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya LABIOFAM ameeleza kuwa Kampuni yake imejipanga na itatekeleza zoezi la uhamishaji wa teknolojia ili Watanzania wapate ujuzi wa kuzalisha bidhaa hizo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!