Home VIWANDAUZALISHAJI Usimamizi thabiti wa madini mkakati utakuza uchumi wa Afrika: Waziri Mavunde

Usimamizi thabiti wa madini mkakati utakuza uchumi wa Afrika: Waziri Mavunde

0 comment 65 views

Waziri wa Madini Anthony Mavunde amezitaka nchi za Afrika wazalishaji wa madini mkakati kuweka usimamizi madhubuti wa rasilimali hizo ili zisaidie kukuza uchumi kwa kuhakikisha unakuwepo mkakakati imara wa kuongeza thamani madini hayo katika nchi wazalishaji.

Mavunde ameyasema hayo Oktoba 02, 2024 wakati akitoa hotuba yake akishiriki Mkutano wa 13 wa Utajiri wa Madini Jijini Kampala, nchini Uganda.

“Kipekee naomba nimpongeze Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni kwa uamuzi wake thabiti wa hivi karibuni wa kukataza usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi.

Hii ni hatua muhimu sana kwa maendeleo ya sekta ya madini na wananchi wa Jamhuri ya Uganda,” amesema Mavunde.


“Sisi Tanzania, tulishafanya uamuzi huo wa kukataza usafirishaji wa madini ghafi nje chini ya uongizi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tumetamka bayana kwamba mwekezaji yeyote atayehitaji kuwekeza kwenye uchimbaji wa madini mkakati ni sharti aoneshe mpango kabambe wa uongezaji thamani nchini Tanzania”, amesisitiza Mavunde.

Aidha, Waziri Mavunde amebainisha, sekta ya madini imeendelea kukua na kufanya vizuri ambapo kwa mwaka 2023, mchango wake kwenye pato la taifa ulifikia asilimia 9. Pia, asilimia 56.2 ya thamani ya mauzo ya bidhaa zote nje ya nchi yalitokana na sekta ya madini, ambapo ilikadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 3.5.

Vilevile, Mavunde amesema kwa upande wa maduhuli, asilimia 60 huchangiwa na wachimbaji wakubwa na asilimia 40 hutokana na wachimbaji wadogo. Hali hiyo imeifanya Serikali ya Tanzania kuendelea kuweka mkazo katika kuwasimamia na kuwaongoza wachimbaji wadogo ili wazalishe kwa tija na kuongeza mchango wao kwenye uchumi wa nchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter