Home VIWANDAUZALISHAJI Waziri Hasunga: Sekta ya kilimo haina sababu ya kutofanikiwa

Waziri Hasunga: Sekta ya kilimo haina sababu ya kutofanikiwa

0 comment 44 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amewataka wataalamu mbalimbali walio katika wizara hiyo kutekeleza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuchochea uzalishaji katika sekta ya kilimo. Hasunga ameeleza kushangazwa na miradi mingi iliyopo katika wizara hiyo, huku ikiwa na uchache wa manufaa.

Waziri Hasunga amesema hayo wakati akifungua kikao kazi cha wakurugenzi wakuu wa bodi za mazao na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo sambamba na wakurugenzi wa bodi za ushauri na wenyekiti wa bodi za wakurugenzi, kikao ambacho lengo kuu lilikuwa ni kufahamiana ambapo washiriki wamepata nafasi ya kueleza jinsi gani kilimo kinaweza kuimarika na kuwa na manufaa kwa wakulima nchini.

“Lazima tuendelee maana rasilimali watu zipo, wasomi wazuri wapo na tafiti zipo hivyo hatuna sababu ya kushindwa kufanikiwa kwenye sekta ya kilimo. Kuna watu wamepewa rasilimali kubwa kwa ajili ya kuzifanyia kazi lakini ufanisi wao na tija katika utendaji ni mdogo sana jambo hili halikubaliki lazima tubadilike”. Amesema Waziri huyo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo amesisitiza kusimamiwa kwa weledi kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika ili kuimarisha sekta ya kilimo hapa nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter