Home WANAWAKE NA MAENDELEO TGNP: Unyanyasaji wa wanawake bado sana

TGNP: Unyanyasaji wa wanawake bado sana

0 comment 68 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi

Na Mwandishi Wetu

Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia nchini (TGNP) Lilian Liundi amesema hadi sasa, bado wanawake wanakumbwa na changamoto ya unyanyasaji wa kijinsia, akiongeza kuwa Mkoa wa Manyara unaongoza kwa vitendo hivyo. Lilian amesema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa anaongea na waandishi wa habari. Amesisitiza kuwa bado nguvu kubwa inahitajika ili kusaidia wanawake kujitambua na jamii kuachana na mila potofu.

Katika kongamano litakalofanyika Septemba 05 hadi Septemba 08 mwaka huu, TGNP watajikita katika kuelimisha wanawake na watoto wa kike ili wapate elimu na nia ya kujikwamua kiuchumi. Lilian ameongeza kuwa wamepanga kuleta wanawake maarufu ili wengine wajionee kuwa bado nafasi ya kujikwamua ipo, hali itakayopelekea wao kufanya makubwa ndani ya jamii.

Mbali na hayo, elimu ya kufanya maamuzi, uwekezaji na ujenzi wa nguvu ya pamoja itatolewa ili wanawake wapate fursa ya kujikomboa kiuchumi. Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na taasisi nyingine binafsi litahudhuriwa na watu takribani 1,000 kutoka mikoa mbalimbali pamoja na viongozi wa serikalini.

Tags:

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter