Home Uncategorized Google yatimiza miaka 21

Google yatimiza miaka 21

0 comment 140 views

Google ni moja kati ya kampuni kubwa na maarufu zaidi duniani. Leo tarehe 27 Septemba mwaka 2019, Google inatimiza miaka 21 tangu kuanzishwa kwake. Bila shaka, Google ina nafasi kubwa katika matumizi yetu ya mtandao na kwa walio wengi, kampuni hii ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Katika kusherekea miaka 21 ya Google, hivi hapa ni vitu kumi na nne (14) ambavyo huenda ulikuwa hufahamu kuhusu kampuni hii maarufu zaidi duniani:

– Google linatokana na neno ‘googol’

– Google ni tovuti inayotembelewa zaidi duniani.

– Google ina angalau siku sita za kuzaliwa lakini inachagua kusherekea tarehe 27 Septemba.

– Makao makuu ya Google yanafahamika kama Googleplex na yanapatikana California Silicon Valley.

– Google ilianzishwa mwaka 1998 na wanafunzi wawili wa chuo ambao walikuwa wakiishi pamoja, Larry Page na Sergey Brin.

– Google ilikuwa kampuni ya kwanza ya teknolojia kuwapa wafanyakazi wake chakula bure kazini na vilevile kuwaruhusu kuleta mbwa wao ofisini.

– Nembo ya kwanza ya Google (Google Doodle) ilitengenezwa mwaka 1998 kwa ajili ya warsha ya Burning Man Festival. Waanzilishi wake (Page na Brin) walitaka watu kufahamu kwanini hawakuwa ofisini.

– Google ilitangaza huduma yake ya barua pepe (Gmail) kwa mara ya kwanza tarehe 01 Aprili mwaka 2004 lakini kwa sababu hii ni siku ya wajinga duniani kote, watu wengi walifikiri kuwa ni utani.

– Google ni mdau mkubwa wa mazingira na kutokana na hilo, makao makuu ya kampuni hiyo hutumia mbuzi wanaozunguka kwenye bustani kutafuta lishe badala la mashine za kufyeka majani.

– Mwaka 1999, Google ilijaribu kuuzwa kwa Dola milioni moja lakini hakuna aliyenunua licha ya bei kushushwa. Leo hii Google inakadiriwa kuwa na thamani ya takribani Dola milioni 300 za Marekani.

– Google inamiliki bidhaa mbalimbali zikiwemo Gmail, Google Docs, Google Drive, Google Translate, Admob, Google Adsense, Google Hangouts, Google Maps na Google Trends.

– Tenzi ‘google’ iliongezwa kwenye kamusi ya Merriam-Webster mwaka 2006 na kutafsiriwa kama kitendo cha kutumia tovuti ya Google kupata taarifa katika mtandao.

– YouTube iliingia rasmi katika familia ya Google mwaka 2006 baada ya kununuliwa kwa Dola za Marekani 1.5 bilioni. Leo hii, mtandao wa YouTube una watumiaji zaidi ya bilioni mbili kwa mwezi.

– Google Image Search ilizinduliwa Julai 2001 kutokana na vazi alilovaa mwanamuziki Jennifer Lopez (Jlo) kwenye tamasha maarufu la muziki la Grammys. Vazi lake lilitafutwa kwa wingi kupitia Google lakini hakukuwa na njia ya kuona picha yake.

Je, wewe ni mtumiaji mkubwa wa Google pamoja na bidhaa zake?

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter