Home BIASHARA Fahamu haya kuhusu huduma kwa wateja

Fahamu haya kuhusu huduma kwa wateja

0 comment 93 views

Huduma bora kwa wateja ni jambo moja wapo la msingi katika biashara yeyote ili kuweza kufanya mauzo zaidi na kupata mafanikio kiuchumi. Kila mwaka duniani huwa kunakuwa na maadhimisho ya huduma kwa wateja, ambayo huadhimishwa wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba ambapo kwa mwaka huu yameanza kuanzia tarehe 7 mwezi huu hadi tarehe 11. Baadhi ya malengo ya maadhimisho hayo huwa ni kuwahamasisha wahudumu katika makampuni na biashara kutoa huduma bora kwa wateja, pia maadhimisho hayo hufanywa ili kuweza kuwakumbusha wateja husika kuwa wao ni muhimu katika kampuni au biashara husika hivyo kuridhika na huduma au bidhaa zinazouzwa ni jambo la muhimu zaidi kwa kampuni au biashara husika ili kuweza kupata maendeleo.

Hivyo basi, kutokana na hayo yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo watu wengi hawafahamu  kuhusu suala zima la huduma kwa wateja:

  • Inaelezwa kuwa ni rahisi kwa wateja kuelezea uzoefu mbaya(huduma mbaya) walioupata katika kampuni au biashara mara mbili zaidi kuliko kushirikisha watu wengine kuhusu uzoefu mzuri(huduma nzuri) walioupata katika kampuni au biashara husika.
  • Inaelezwa kuwa ni asilimia 4 tu ya wateja hulalamika, huku wateja 26 licha ya kutofurahishwa na huduma wateja hao huamua kukaa kimya.
  • Pia inaelezwa kuwa hadi kufika 2020, 85% ya wateja watafanya mahusiano ya kibiashara na wafanyabiashara bila ya kuonana ana kwa ana.
  • Ni rahisi kwa mteja kununua bidhaa kwa mshindani ( kwa mara nne) ikiwa tatizo ni huduma katika sehemu ya mwanzo aliyotaka kufanya manunuzi na si suala la bei au bidhaa zinazohusiana katika kampuni husika.
  • Ili kuweza kumfanya mteja asahau uzoefu mbaya (huduma mbaya) aliyopata mara 1, mteja huyo hutakiwa kupata uzoefu mzuri si chini ya mara 12 ili kuweza kuendelea kununua bidhaa au huduma katika kampuni husika.
  • Vile vile inaelezwa kuwa 74% ya wateja hubadilisha brand ikiwa wanaona mchakato wa ununuzi ni mgumu sana.
  • Kupitia tovuti ya Newvoicemedia.com imeelezwa kuwa 51% ya wateja huwa hawaendelei kufanya biashara na kampuni au biashara ambayo walipata uzoefu mbaya(huduma mbaya) kwa mara ya kwanza.
  • 77% ya wateja hupendekeza kampuni husika kwa marafiki na ndugu ikiwa watapata huduma na uzoefu mzuri kupitia kampuni hiyo.
  • Zaidi ya 95% ya wateja wanaweza kuendelea kufanya manunuzi katika kampuni husika ikiwa malalamiko yao yatafanyiwa kazi kwa uharaka na matokeo yakawa ya kuridhisha.
  • 80% ya makampuni husema kuwa wanatoa huduma ya hali ya juu, huku watu 8% wanafikiria kuwa ni kweli kuwa kampuni hizo zinatoa huduma za hali ya juu kwa wateja.

Kwa ujumla, yapo mambo mengi ambayo wafanyabiashara wanatakiwa kujifunza na kuboresha ili kuweza kuhakikisha wateja wanaridhika kila wanaponunua huduma au bidhaa husika zinazouzwa. Ili kuhakikisha huduma kwa wateja ni ya hali ya juu ni muhimu kupata mafunzo kuhusu mchakato mzima wa utoaji wa huduma kwa wateja ili kuweza kujifunza na kwenda sawa na mabadiliko yanayofanyika duniani kila siku hususani katika upande wa  teknolojia kulingana na aina ya wateja kampuni inayojihusisha nayo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter