Mbali na Watanzania wengi hasa vijana kuamua kujiajiri kutokana na uhaba wa ajira nchini, bado vijana wengi wako mitaani na wana uhitaji wa ajira ili waweze kujikwamua kimaisha kwani si kila mtu lazima awe mjasiriamali. Hivyo basi hapa chini ntataja tovuti 3 maarufu ambazo zimewasaidia watu wengi kupata ajira na kuweza kubadilisha maisha yao katika upande wa kipato na uchumi. Tovuti hizo ni:
Ajira yako
Kupitia tovuti hii mtu yeyote anaweza kuona nafasi za kazi kutoka katika kampuni mbalimbali zilizopo nchini (za kiserikali na zisizo za kiserikali). Nafasi hizo za kazi hutangazwa kila siku hivyo kuleta urahisi wa kujua kazi husika imetangazwa lini, na kama muda wa tangazo hilo umeisha au la. Pia kupitia matangazo ya kazi hiyo inasisitizwa kutotoa malipo yeyote kwani watu wengi wametapeliwa kutokana na matangazo yasiyo ya kweli ambayo huwataka watu kufanya malipo ili kuweza kuomba kazi husika.
Bonyeza link hii kupata maelezo na taarifa zaidi kuhusu tovuti hii: https://www.ajirayako.co.tz/
Brighter Monday
Kupitia tovuti hii mtu yeyote anayetafuta kazi au watu wa kuajiri ana uwezo wa kutafuta na kupendekezewa ajira/waombaji wa kazi wanaoendana na matakwa yake. Pia kupitia tovuti hii hakuna haja ya kutengeneza CV kila wakati, kwani baada ya kutengeneza CV kupitia tovuti hii basi utatumia CV hiyo hiyo kila mara itakavotokea kuna kazi unataka kuiomba. Aidha watumiaji wa tovuti hii hupata ushauri kuhusu masuala ya ajira ili kuweza kujiboresha na kuwa waombaji wenye vigezo zaidi, hii husaidia katika kupata kazi stahiki kutokana na ujuzi na utaalamu wa mtu husika.
Bonyeza link hii kupata maelekezo,taarifa na hata kutafuta kazi au mfanyakazi kupitia tovuti hii: https://www.brightermonday.co.tz/
Ajira zetu
Tovuti hii pia haina tofauti na tovuti nlizotaja hapo juu, ambapo kupitia tovuti hii watu wanaweza kutafuta kazi au makampuni na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali zinaweza kutangaza kazi ili kuweza kutoa ajira. Pia ikiwa mtu ana maswali kuhusu jambo lolote, baada ya kufungua tovuti hiyo huwa kuna ujumbe unakuja ambao humuwezesha mtu kuuliza na kujibiwa maswali moja kwa moja mara baada ya kuandika jina na barua pepe yake.
Ili kujua zaidi kuhusu tovuti hii bonyeza hapa: https://www.ajirazetu.co.tz/
Aidha kupitia mtandao wa intaneti watu wamepata ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi. Hivyo ni muhimu kupitia tovuti, blogu, mitandao ya kijamii kama instagram, facebook, LinkedIn nk ili kuweza kupata kazi ambayo unaweza kuimudu kulingana na ujuzi na utaalamu ulio nao.
Pia inasisitizwa kwa kila muombaji wa kazi kuwa na kitambulisho cha kitaifa kinachotolewa na NIDA ili kuweza kuomba kazi katika taasisi,mashirika na kampuni mbalimbali kwa urahisi, kwani bila kitambulisho hicho mchakato wa uombaji unaweza usikamilike.