Home BIASHARA Unataka wateja wakufikie kwa urahisi kupitia Google maps?

Unataka wateja wakufikie kwa urahisi kupitia Google maps?

0 comment 112 views

Teknolojia imerahisisha ufikaji wa maeneo mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na maeneo ya biashara, katika makazi ya watu nk. Ramani ya Google au maarufu kama ‘Google Maps’ imekuwa ni msaada mkubwa kwa wateja kujua maeneo ambayo wanaweza kupata bidhaa au  huduma fulani na kwa upande wa wamiliki wa biashara imewasaidia kupata wateja zaidi kwani mbali na kupata taarifa ya eneo husika la biashara mteja huweza kuona picha, na video kuhusu bidhaa au huduma husika jambo ambalo huvutia wateja wengi kununua bidhaa au huduma hiyo.

Mambo ya kufanya ili kuweza kuweka taarifa za biashara yako katika Google maps;

Akaunti ya Gmail

Jambo la kwanza unalohitaji ili kuweza kuorodhesha biashara yako Google maps ni akaunti ya gmail. Kutengeneza akaunti ni bure, ni muhimu kujaza taarifa za ukweli kuhusu biashara yako katika akaunti ya gmail kwasababu taarifa hizo ndio zitakazotumika katika google maps. Pia hakikisha unatengeneza neno la siri (password) ya kipekee ili kuhakikisha usalama wa akaunti wakati wowote. Ikiwa unataka kutengeneza akaunti ya gmail tembelea link ya Gmail.com.

Kujisajili katika programu ya Google maps

Hakikisha una programu ya google maps katika simu yako, ni bure kupakua programu hii kupitia Play store kwa simu za  Android na App store kwa simu za iOS . Baada ya kupakua programu hiyo hakikisha umewasha ‘location yako, kisha ingia kwenye programu ya google map upande wa kushoto juu kabisa utaona mistari mitatu bonyeza hapo na kushuka chini hadi utakapoona maneno yanasema ‘add a missing place’ kisha bonyeza maneno hayo. baada ya kubonyeza maneno hayo ukurasa mpya utafunguka hapo ndio sehemu ya kujaza taarifa za biashara yako. Baadhi ya taarifa ambazo unatakiwa kujaza kuhusu biashara yako ni pamoja na eneo biashara ilipo, muda wa kufungua na kufunga biashara, namba ya simu, linki ya tovuti ya biashara na kuweka picha zinazoelezea biashara husika kisha bonyeza ‘send’ kukamilisha mchakato wa kujisajili.

Baada ya kukamilisha usaili wa taarifa za biashara yako, google itahitaji kudhibiti habari ulizotoa. Hivyo utapokea barua  kutoka google ambayo itatoa maagizo ya kina ya kudhibiti orodha yako. Mara tu mchakato huo utakapokamilika (mara nyingi hukamilika ndani ya masaa 24) basi taarifa kuhusu biashara yako zitaonekana katika programu ya google maps.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter