Home BIASHARA Njia tatu za uhakika zilizothibitishwa za kuwapiku wenzako kibiashara

Njia tatu za uhakika zilizothibitishwa za kuwapiku wenzako kibiashara

0 comment 176 views

Sio rahisi kuanza kuanzisha biashara yako bila kutokuwepo ama ikakosekana biashara inayofanana ama ina uwiano na hiyo/hizo,ila unaweza tumia njia tatu muhimu kuwapiku wengine na hata kujiongezea kipato zaidi.

Punguza gharama

Punguza gharama za matumizi yako binafsi ili tu yasije athiri biashara zako.Usipunguze mishahara ya wafanyakazi au gharama za manunuzi ya bidhaa bali punguza gharama za uendeshaji zisizo kua na tija ama faida katika biashara yako.

Kua mbunifu

Baada ya kufanya tathmini ya soko na kugundua siri ya ushindi,fahamu ni mbinu gani za kipekee utakazozitumia kuwafikia wateja wako.Unaweza ukaanza utaratibu wa kuwapelekea wateje wako bidhaa mpaka nyumbani kama wenzako maeneo uliyopo hawatoi huduma kama hiyo.

Toa huduma zipitazo matarajio ya wateja wako

Kuwapa huduma nzuri wateja wako kutawafanya warudi tena na hata kua mabalozi wa biashara yako kwa wateja wengine,zingatia lugha nzuri na pia kubali maoni pale watakapo kushauri jambo zuri kuhusiana na biashara yako.

Kwa kuzingatia hayo hakika utaona mabadiliko ya biashara yako na hata uwezekano wa kukuingizia kipato kwa haraka

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter