Home Elimu Kuweka akiba kwa ajili ya masomo

Kuweka akiba kwa ajili ya masomo

0 comment 137 views

Katika kila jambo unalo fanya ama kulipangilia lazima uweke malengo pia ujue ni njia gani hasa unazotakiwa kuzifanya ili tu uweze kutimiza malengo yako.

Kwenye kila kipato unachoingiza,hakikisha kuna asilimia uliyojiwekea na hupaswi kuitumia hiyo asilimia kwa shughuli nyingine yoyote,bali unapaswa kutunza asilimia hizo pembeni maalum kwa ajili ya uwekezaji au malengo ya kuitumia pesa hiyo ili tu ikusaidie kwa ajili ya chuo.

Unapopata fedha,kabla hujaanza kulipa bili mbalimbali unazodaiwa au kununua vitu unavyohitaji,jilipe wewe mwenyewe kwanza,hii ni tabia moja rahisi ambayo imewawezesha wengi kufikia malengo yao,bila kujali kiasi cha kipato walichonacho.Unapaswa Kwanza kabla hujafanya matumizi,kwa sababu ukisema utumie halafu itakayobaki ndio utunze,hutabakiwa na kitu.

Zoezi la kufanya;katika kila kipato unachooingiza,kabkla hujaanza kupangilia unakitumiaje ,ondoa kwanza asilimia kadhaa ya kipato hicho na weka pembeni,weka mahali ambapo hutokitumia hata iweje.Kipato hicho ni kwa ajili ya masomo yako,na ndichioo kipato kitakachokufanya wewe ukatimiza ndoto zako za kujilipia kwa ajili ya masomo yako.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter