Home AJIRA CORONA ITASABABISHA WATU MILIONI 200 KUPOTEZA AJIRA DUNIANI

CORONA ITASABABISHA WATU MILIONI 200 KUPOTEZA AJIRA DUNIANI

0 comment 103 views

Asilimia 81 ya wafanyakazi wote duniani, sawa na watu bilioni 3.3 wameathirika na janga la virusi vya corona baada ya sehemu zao za kazi kufungwa kabisa ama kwa kiasi.

Marufuku kadhaa na mabadiliko ya lazima maisha ya kila siku yamesababisha kufungwa kwa makampuni mengi ulimwenguni na kuwarudisha nyumbani wafanyakazi wake – aidha moja kwa moja ama kwa muda.

Shirika la Kazi Duniani (ILO), limekuwa likifuatilia madhara ya janga hili katika sekta ya ajira na kuandaa taarifa mbalimbali zinaoonesha ukubwa wa tatizo ulimwenguni kote.

“Wafanyakazi na wafanyabiashara wanakabiliwa na janga kubwa, na hiyo ni kwa nchi tajiri na masikini,” ameeleza mkurugenzi mkuu wa ILO Guy Ryder.

“Inabidi twende kwa pamoja kwa mwendo wa haraka na malengo maalumu. Hatua sahihi na za haraka zinaweza kuamua utofauti wa kustahamili hali hii ama kuanguka kabisa.”

Mlipuko wa virusi vya corona unatazamiwa kukata asilimia 6.7 ya saa za kazi duniani kote katika robo ya pili ya mwaka 2020.

Hiyo ni sawa na wafanyakazi wa ajira za kudumu milioni 195 kupoteza ajira zao.

Ukanda unaotizamiwa kuathirika zaidi ni nchi za Arabuni kwa kupungua kwa asilimia 8.1ya saa za kazi (sawa na wafanyakazi milioni tano wa kudumu).

ILO inase a hili ni “janga baya zaidi ” toka kwisha kwa Vita ya Pili ya Dunia.

Pia inaonya kuwa kuongezeka kwa kiwango cha watu wasio na ajira duniani kwa mwaka 2020 kitapanda kutokana na sababu kuu mbili:

  • § Kasi ya uchumi wa dunia katika kurejea katika mstari katika nusu ya pili yam waka 2020.
  • § Namna gani sera zitakuwa madhubuti na kuchochea kukua kwa nafasi za ajira.

Kuna hatari ya kuwa takwimu za mwisho wa mwaka zitakuwa kubwa kuliko makadirio ya awali ya watu milioni 25.

Sekta za malazi na viwanda zaathirika vibaya

Sekta tofauti za uchumi zimeathirika kwa namna za tofauti pia kutokana na kupungua ama kusimama ghafla kwa shughuli za uzalishaji.

Si ajabu, kukiwa na safari za chini kabisa na maisha ya kawaida yakivurugika sekta ya malazi na chakula (hoteli na migahawa) ni moja ya zile ambazo zimeathirika zaidi, pamoja, viwanda na biashara za mauzo ya jumla na rejereja na biashara ya kujenga, kuuza na kupangisha nyumba.

Sekta hizo zote kwa pamoja ni sawa na asilimia 38 ya kazi zote duniani huku zikiajiri watu bilioni 1.25.

Marekani na Ulaya kuna wafanyakazi wengi walio hatarini

Wastani wa watu ambao wanafanya kazi zilizo hatarini kupotea unatofautiana ulimwenguni.

Jumla ya asilimia 43.2 ya watu wa Amerika ya Kusini na Kaskazini na asilimia 42.1 Ulaya na Asia ya kati wanafanyakazi katika sekta zilizomo hatarini.

Maeneo hayo yana wafanya kazi wachache ambao wapo kwenye zisizo rasmi ambao hao ndio wengi barani Afrika, Arabuni, sehemu kubwa ya Asia na Pasifiki.

Japo wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi wanachangia sehemu kubwa ya kukua kwa uchumi katika nchi kama India, Nigeria na Brazili, lakini hawapati faida kama hifadhi ya jamii ambazo wafanyakazi wa sekta rasmi wanapata.

Kwa Afrika asilimia 26 ya watu wanafanya kazi katika sekta zilizomo hatarini.

“Huu ni mtihani mkubwa kwa ushirikiano wa kimataifa kwa zaidi ya miaka 75. Endapo nchi moja itafeli, basi wote tutafeli. Lazima tutafute njia za kukwamua kila sehemu ya jamii yetu ya kimataifa, hususani wale ambao wanaweza kupata madhara zaidi ama hawawezi kujikwamua,” ameeleza mkuu wa ILO bw Ryder.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter