Home BIASHARA NAMNA UNAVYOWEZA KUBANA MATUMIZI KATIKA BIASHARA

NAMNA UNAVYOWEZA KUBANA MATUMIZI KATIKA BIASHARA

0 comment 137 views

Biashara bado inaendelea kuwa moja kati ya sekta muhimu za maendeleo. Mtu yeyote anayefanya biashara anawaza kunufaika na kufanikiwa kimaisha kupitia biashara hiyo. Hasara haikosekani katika biashara lakini ni vema zaidi kuchukua tahadhari kabla ili kuepukana na hasara.

ADVERTISEMENT

Watu wengi wamekuwa wakianzisha biashara pasipo kuangalia ukubwa au udogo wa biashara zao na namna ya kuendesha biashara zao ili ziwe zenye kuwaletea faida zaidi. Moja ya vitu vitakavyofanya biashara yako kukua ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji.

Unafanyaje ili kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara yako? Zipo njia kadhaa ambazo mjasiriamali au mfanyabishara anaweza kufanya ili kutengeneza faida zaidi kwa kuondoa gharama zisizo za lazima katika uendeshaji kama vile:

  1. Kupitia gharama za mapato na matumizi ya biashara yako. Biashara nyingi zimeshindwa kusonga mbele kutokana na walio wengi wa wafanyabiashara hao kutopitia mapato na matumizi ili kujipa tathmini ya biashara zao. Kuipitia biashara yako kunasaidia kukupa dira na muelekeo.
  2. Kufanya manunuzi karibu na eneo la huduma/biashara. Hii itasaidia kuondoa gharama kubwa za usafirishaji wa bidhaa au vifaa kutoka sehemu moja hadi nyingine, kujihakikishia uwepo wa akiba ya kutosha sambamba na kujijengea ukaribu na kampuni zinazohusiana na mauzo ya bidhaa hizo na kwa kufanya hivyo inatengeneza mazingira ya kufanyiwa punguzo kila unaponunua bidhaa au vifaa.
  3. Hamasisha uzalishaji kwa wafanyakazi. Wasaidie wafanyakazi wako kuwa wajuzi wa taaluma zaidi ya moja na kama itawezekana wekeza kiasi cha fedha kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya ujuzi mbalimbali.
  4. Punguza Matumizi yasiyo ya lazima. Matumizi madogo madogo yanaweza kuchangia hasara kubwa katika biashara zako.
  5. Epuka kuajiri wafanyakazi pasipo na ulazima na punguza idadi ya nguvu kazi inapobidi. Kuna haja kubwa ya kuondoa wale wafanyakazi wasio na ulazima sana ili pesa ambayo    ingetumika kuwalipa itumike katika kuwekeza sehemu nyingine.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter