Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema,Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo zinapaswa kuwa na mkataba wa huduma kwa Wateja ili kurahisisha utoaji wa huduma boara kwa wanannchi.Hayo ameyasema Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi jijini Dar es Salaam wakati akizindua mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), amesema kuwa TMDA imekuwa na mipango mizuri katika utoaji wa huduma kwa kuzingatia muda katika utoaji wa leseni kwa wadau mbalimbali.
Profesa Makubi amesema kuwa TMDA imekuwa na mifumo ya viwango ambapo Shirika la Afya Duniani inatambua pamoja na jumuiya mbalimbali na hiyo inatokana na mikakati ya watendaji wa taasisi waliojiwekea ya kuhakikisha wanakwenda kutatua matatizo ya huduma katika utoaji wa huduma.
Amesema kuwa TMDA inatoa mkataba mara ya nne ambapo amewataka mamlaka hiyo kufuatilia mkataba huo kuona malengo waliojiwekea yameweza kama wameweza waliojipangia pamoja na huduma wanazozitoa kwa wadau.
kwa wadau amesema TMDA tangu walipoanza kutengeneza mkataba wa huduma kwa wateja wamekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma bora kutokana na watendaji kujipanga katika kuhudumia wateja hao.