Home BIASHARA Sukari ya magendo yaua soko la viwanda vya ndani

Sukari ya magendo yaua soko la viwanda vya ndani

0 comment 127 views
Na Mwandishi wetu

Kutokana na kukithiri kwa biashara ya sukari ya magendo kutoka nchini Kenya, soko la viwanda vya ndani kikiwemo kiwanda cha sukari cha TPC kilichopo Moshi limeanza kupata changamoto. Ofisa MtendajiMkuu na Utawala wa TPC Jaffary Ally amedai kuwa sukari hiyo ya magendo imepoteza soko la TPC kwa takribani asilimia 30 hadi sasa.

Akitolea ufafanuzi juu ya suala hilo wakati wa kikao cha wafanyabiashara na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ili kujadili fursa za uwekezaji na ushiriki wa sekta binafsi, Jaffary amedai kuwa sukari hiyo imekuwa ikizagaa mitaani baada ya kuingizwa hapa nchini kupitia njia zisizo halali katika wilaya za Rombo, Kilimanjaro na mkoa wa Tanga.

Jaffary amemuomba Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kutizama suala hili kwa undani zaidi. Mbali na hayo, ameshauri serikali kupitia upya changamoto ya ushuru wa mazao (CESS Leavy) ambayo hutozwa na Halmashauri za wilaya kwani hazitambui msamaha wa kodi hiyo kama Sheria ya EPZA ilivyoelekeza.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter