Home FEDHA Umaskini bado ni tatizo nchini: Waziri wa Fedha

Umaskini bado ni tatizo nchini: Waziri wa Fedha

0 comment 101 views

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Phillip Mpango amesema ingawa Tanzania imeweza kuingia katika uchumi wa kati, umaskini bado ni tatizo nchini.

Dk Mpango alisema hayo Novemba 16 katika sherehe za kuapishwa jijini Dodoma.

“Ingawa tumefanikiwa kuingia uchumi wa kati, kiwango cha umaskini bado kipo juu, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu tumeshuhudia wananchi wetu wakiwa na uhitaji,  bado tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii kuwanyanyua watu wetu,” alisema waziri Dk Mpango.

Dk Mpango na Prof Palamagamba Kabudi wamekuwa mawaziri wa kwanza kuteuliwa na Rais John Magufuli katika baraza lake jipya la mawaziri na waliapishwa jana jijini Dodoma pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter