Home BIASHARA Sekta ya mifugo na uvuvi inufaishe wananchi: Waziri Ndaki

Sekta ya mifugo na uvuvi inufaishe wananchi: Waziri Ndaki

0 comment 157 views

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imesema itahakikisha inawaondoa wananchi katika umaskini, kupata ajira kupitia sekta za mifugo na uvuvi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki alisema wizara hiyo inachukulia kwa uzito mkubwa suala la viwanda, hivyo inataka kubadilisha fikra za wavuvi na wafugaji.

Alisema “wananchi wetui wapate ajira, waondokane na umaskini na sisi tuuze bidhaa za mazao ya uvuvi na mifugo yaliyo bora hapa ndani na kwa wenzetu nje, sasa mimi nikikuta hali ya mkwamo kwa kitu ambacho kinatusaidia kuelekea huko napata shida”.

Waziri Ndaki alisema kama ilivyo katika sekta nyingine, sekta ya uvuvi ni muhimu kwa uchumi wa nchi na inatakiwa kuchukuliwa kwa uzito.

“Tunalichukulia kwa uzito suala la viwanda, ndio maana serikali ya awamu ya tano imelipa kipaumbele na tunaamini kwamba litasaidia kubadilisha fikra za wafugaji na wavuvi badala ya kufanya kazi zao kwa mazoea, watafanya kwa kulenga biashara zaidi kwa kutumia fursa ya uwepo wa viwanda ili kujiongezea kipato,” alisema.

Aliongeza kuwa bado kunahitajika kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo.

Aliwataka wawekezaji wa viwanda vya samaki mkoani mwanza kutumia usafiri wa ndege kutoka Mwanza kusafirisha minofu ya samaki kwa wingi ili kutangaza zaidi bidhaa hiyo duniani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter