Home BIASHARA Sh500, mjasiriamali kupata eneo kufanya mnada kituo cha daladala Mawasiliano

Sh500, mjasiriamali kupata eneo kufanya mnada kituo cha daladala Mawasiliano

0 comment 83 views

 

Fursa imetangazwa kwa wajasiriamali jijini Dar es Salaam kuchangamkia mnada wa kila siku za ijumaa ulionza leo Januari 8, 2021 katika kituo cha daladala cha Mawasiliano Simu 2000.

Meneja wa Kituo hicho, Geofrey Mbwama amesema wameanzisha gulio hilo stendi hapo ili kuleta chachu kwa watu wanaoingia kituoni hapo kujua kuwa kuna soko la kupata mahitaji mbalimbali.

Amesema “tumekuja na hili wazo la gulio la kila ijumaa ili kuwasidia wajasiriamali wetu wa  Dar es Salaam, hivyo tunawakaribisha wote na wakifika hapa watapangiwa sehemu kwa kulipia ushuru wa Sh 500 tu.
Mbwama ameongeza kuwa “iwapo mtu atahitaji sehemu ya kudumu basi ataonana na ofisi ya Meneja wa kituo”.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter