Home BIASHARA Tusitumie sheria na makosa kama kitega uchumi: Rais Samia

Tusitumie sheria na makosa kama kitega uchumi: Rais Samia

0 comment 122 views

Rais wa Tanzania, Samia Hassan amelitaka Jeshi la Polisi kutojielekeza kutumia sheria na makosa barabarani kama kitega uchumi chake  badala yake wajielekeze kutoa elimu.

Rais Samia ameeleza hayo leo Jumanne Mei 18, 2021 katika uzinduzi wa kiwanda cha ushonaji katika bohari kuu ya jeshi la polisi nchini kilichopo eneo la Kurasini, Dar es Salaam kilichojengwa kwa Sh milioni 666.4.

Amesema ni vyema polisi kuongeza jitihada za utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya usalama barabarani kama inavyofanyika sasa ili wasikie na waelewe.

Rais amesema “ni vyema kwa sababu najua kiwanda hiki kimejengwa kwa pesa hizo, lakini ni vyema tukajielekeza kwenye elimu zaidi kuliko kuzitumia sheria kama vitega uchumi”.

Akizungumza katika uzinduzi huo, mkuu wa jeshi la polisi (IGP), Simon Sirro amesema takribani Sh50.1 bilioni zimekusanywa na polisi kutokana na makosa ya tozo za usalama barabarani kati ya Julai 2020 hadi Aprili 2021.

Amesema fedha hizo ni pungufu ikilinganishwa na Sh56 bilioni zilizokusanywa kati ya Julai 2019 hadi Julai 2020 huku sababu ikitajwa kuwa watu sasa wameanza kuwa watii wa sheria.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter