Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mokgweetsi Masisi anatarajia kuzuru Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia kesho Juni 10, 2021 kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula amesema Rais Masisi atawasili nchini kesho asubuhi na baada ya hapo atakuwa na mazungumzo ya mwenyeji wake Ikulu Jijini Dar es Salaam.
“Viongozi wetu wanatarajia kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, uhusiano wa kidiplomasia, matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini Botswana, bishara na uchumi pamoja na namna ya kuimarisha zaidi Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc),” amesema.
Balozi Mulamula amesema Rais Masasi ataondoka nchini Ijumaa Juni 11, 2021.