Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Wananchi Dar watakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona

Wananchi Dar watakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona

0 comment 101 views

Kufuatia kuwepo kwa viashiria vya mlipuko wa ugonjwa wa Corona, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari na kuziagiza Taasisi na sehemu zote za mikusanyiko kuweka ndoo za maji na miundombinu ya maji tiririka.

Akitoa tahadhari hiyo, RC Makalla amesema kutokana na mwingiliano wa watu kutoka nchi jirani na mikoa mingine wameona ni vyema kutoa tahadhari kwa wananchi.

Miongoni mwa tahadhari ambazo RC Makalla amewataka Wananchi kuzichukuwa ni pamoja na kuvaa kwa usahihi barakoa (mask) kila wawapo sehemu za mikusanyiko ikiwamo vyombo vya usafiri, masoko, sherehe, maofisini na vituo vya afya.

Kunawa Mikono kwa Maji tiririka na sabuni, kuwahi mapema vituo vya afya wanapobaini dalili za Corona ikiwemo homa Kali, mafua, kikohozi na uchovu.

RC pia amewaasa wananchi kufanya mazoezi ili kuimarisha kinga ya mwili, kula mlo kamili.

Aidha RC Makalla amewaelekeza wakuu wa Wilaya, wakuu wa taasisi za umma na za kiraia na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maelekezo hayo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter