Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, watu wenye ujuzi wa hali ya juu Tanzania ni 3.3% peeke huku wenye ujuzi wa kati wakiwa ni 17%.
Kipanga ametoa takwimu hizo wakati akifunga maonyesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Tecknolojia na kusema “taasisi zetu za elimu ya juu bado zina kazi kubwa ya kuongeza wataalamu wa kiwango cha ujuzi wa juu na wa kati.”
Hii inaonyesha kwamba taasisi zetu za elimu ya juu bado zina kazi kubwa ya kuongeza wataalamu wa kiwango cha ujuzi wa juu na wakati.
Amesema ushiriki wa wanafunzi wa Tanzania katika elimu ya juu kwa sasa ni 6.1% ambapo bado tupo nyuma ya wastani wa Nchi za Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara wa 9.4%. na pia tupo nyuma ya majirani zetu wa Kenya ambao kwa takwimu za mwaka 2018 walikuwa na washiriki kwa asilimia 11.
Wastani huu bado upo chini sana hivyo muhimu kuendelea kuweka mipango itakayoongeza idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu wenye ujuzi na maarifa yanayotakiwa sokono.