Home BIASHARA Waziri Nape: kama unaamini umeibiwa kifurushi leta ushahidi

Waziri Nape: kama unaamini umeibiwa kifurushi leta ushahidi

0 comment 156 views

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kwamba uchunguzi uliofanya na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) umebaini kuwa hakuna wizi wa vifurushi vya mawasiliano ya simu unaofanywa.
Waziri Nape amesema, kuna changamoto mbili kubwa kwenye matumizi ya simu janja ambapo, kwanza, mtumiaji anaweza kujiunga kifurushi cha intaneti, licha ya kuwa hatumii simu, kikapungua au kuisha kwa sababu kuna programu zinazoendelea kujiendesha kwenye simu.
Ametaja changamoto ya pili kuwa matumizi ya ‘hotspot’ ambapo uchunguzi wa TCRA umebaini kuna watu wamekuwa wakitumia huduma ya hotspot kwenye simu za watu wengine, hivyo kupelekea vifurushi vyao kuisha kwa wakati.

“Yeyote anayeamini kaibiwa kifurushi kabla hajatumia akakuta kimeisha, alete ushahidi tutafanya uchambuzi kwa kutumia vifaa vya kisasa natutaweka hadharani kuonyesha tatizo lilipo. Lakini mpaka leo malalamiko yote yaliyopokelewa tatizo limekutwa ni uelewa wa matumizi ya simu janja,” Waziri Nape.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma Waziri Nape amebainisha kuwa elimu zaidi inahitajika juu ya matumizi ya intaneti na simu janja, na kwamba hakuna wizi wowote unaofanywa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter