Home VIWANDANISHATI Tutaendelea kutoa ruzuku kwenye mafuta mpaka duniani kukae sawa

Tutaendelea kutoa ruzuku kwenye mafuta mpaka duniani kukae sawa

0 comment 132 views

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kukata Sh bilioni 100 kila mwezi kwenye matumizi ya serikali ili kuweka ruzuku kwenye mafuta mpaka bei ya bidhaa hiyo itakapo kaa sawa.

“Tunachofanya serikali, tunajaribu kutoa ruzuku kama mlisikia mwezi uliopita nilisema natoa ruzuku ya bilioni 100 kufidia kwenye mafuta ili bei zishuka, na mwezi huu bei zimeanza kushuka polepole.

Tutaendelea kutoa hiyo ruzuku mpaka duniani kukae sawa, kwa hiyo zitakuwa zinashuka sio kwa kiasi kikubwa lakini zitashuka mpaka tufikie pale ambapo bei zitarudi kama zilivyokuwa.”

Rasi Samia amesema serikali itaendelea kukata fedha hiyo kila mwezi mpaka bei zikae sawa ikiwa ni kupunguza makali ya upandaji wa bei za mafuta.

“Mafuta ni janga la ulimwengu ndugu zangu, naomba tuelewane hivyo na wala sio janga la serikali, ni ulimwengu mzima uko hivyo.

Rais Samia amesema hayo alipokua njiani akielekea Kagera kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu inayoanza tarehe 08 Juni, 2022.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter