Home BIASHARAUWEKEZAJI Biashara ya makaa ya mawe kuinua uchumi

Biashara ya makaa ya mawe kuinua uchumi

0 comment 233 views

Biashara ya Makaa ya Mawe inatarajia kuleta tija kwa Watanzania kutokana na uhitaji mkubwa wa madini hayo ndani na nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa ameeleza hayo Novemba 12, 2022 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma alipotembelea mgodi wa uchimbaji wa Makaa ya Mawe wa Ruvuma Coal Ltd.

Dk. Kiruswa amesema serikali imeweka mazingira wezeshi ya uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayovutia wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani kuja kuwekeza na kufanya biashara ya madini mbalimbali yakiwemo makaa ya hayo.

Ameongeza kuwa, serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa makaa ya mawe kutoka kwenye migodi hususan barabara ya kuelekea mkoani Mtwara ili kusafirisha makaa ya mawe bandari.
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza Mangosongo amesema, kutokana na uwepo wa migodi imesaidia wilaya hiyo kupata faida nyingi katika kutekeleza shughuli za kijamii ikiwemo ujenzi wa shule na vituo vya afya.

Naibu Waziri alitembelea mgozi huo kujionea shughuli za uchimbaji zinazoendelea katika mkoa huo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter