Home BIASHARA Bei zitapungua mwezi Machi: Bashe

Bei zitapungua mwezi Machi: Bashe

0 comment 120 views

Serikali imesema bei ya vyakula nchini zitashuka kuanzia Machi mwaka huu.

Kumekuwa na upandaji wa bei za vyakula nchini ambapo bei ya kilo moja ya unga imefikia kati ya Sh2000 hadi Sh2500 huku bei ya kilo moja ya maharage imefikia Sh4000 hadi Sh4500.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema bei hizo zitashuka na kuwapunguzia wananchi gharama za maisha wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Januari 10, 2022 mkoani Dodoma.

Bashe amesema “nikiri kwamba ni kweli tuna changamoto za bei za vyakula lakini ni kipindi cha mpito na baadaye bei zitashuka, na siyo kwamba wizara ya kilimo hatuelewi upandaji bei za vyakula.”

Kama waziri naweza kusema kwamba bei ya chakula itashuka kuanzia Machi hadi April kwani vyakula vitakuwa vingi.”

Ametaja kitaja gharama za usafirishaji kama moja ya sababu inayochangia kupaa kwa bei.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter